
Msingi wa kukata kiuno.Kama nilivyosema awali, simama wima na jishike kiunoni (kuhu na huku) kisha peleka sehemu ya kiuno ya kulia upande wa kulia, sehemu ya mbele ipeleke mbele uwezavyo (nina maana ile pelvis tu sio tumbo na kila kitu) alafu baada ya hapo peleke sehemu yako ya kiuno ya kushoto upande wa kushoto, kisha peleka sehemu yako ya mbele nyuma hali itakayofanya matako yako yabinuke na kujitokeza kwa nyuma. Nyoosha magoti kisha rudi kulia (ulipoanzia). Fuata hatua hizo kwa mara nyingine tena ambazo ni simama wima kisha peleka kiuno kulia, mbele, kushoto, nyuma, kulia mara 20 na kuendelea inategemea zaidi na bidii yako.Baada ya kuzoea hatua hizo hapo ndio unapotakiwa kutengeneza mirindimo yako kivyako. Mfano lala chali, kifudifudi (lalia tumbo), ubavu, chutama, piga magoti n.k kisha peleka kiuno kulia, mbele, kushoto, nyuma, kulia mpaka kiuno kizoee.
Kidokezo: Zoezi zuri la kukata kino ni kulala kifudifudi (kulalia tumbo) kisha kukizunguusha.