
MWANADADA mwenye sauti tamu kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amesema katika maisha yake kamwe hafikirii kuja kuolewa na mwanaume mfupi kwani siyo sampuli yake.

“Nisiongee uongo kusema eti sipendi kutoka kimapenzi na mwanaume mfupi wakati nilishawahi kufanya hivyo na siwezi kujiapiza katika hilo, ila kwenye swala la ndoa lazima nizingatie kigezo changu muhimu cha kuolewa na mwanaume mrefu,” alisema Linah.